MREMA-UHAKIKA WA MAENDELEO KATA YA MLANGARINI NI LAZIMA,AANZA KUISUKA KWA KISHINDO BARABARA KUPITIKA MUDA WOTE

DIWANI MREMA ATOA AHADI KWA WANANCHI WA KATA YA MLANGARINI

Na Joseph Ngilisho-ARUMERU


DIWANI wa Kata ya Mlangarini,katika halmashauri ya Arusha dc ,Emmanueli Mrema, amesema amepokea kwa unyenyekevu na shukrani kubwa dhamana aliyopewa ya kuwatumikia wananchi wa Mlangarini na Wilaya ya Arumeru kwa ujumla na kuahidi kuanza utekelezaji wa ahadi zake mara moja.

Akizungumza leo Dec 2,2025 mara baada ya kuapishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri  ya Arusha DC, Mrema alisema uteuzi na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wananchi ni jambo linalompa nguvu ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kujituma.

> “Nimepokea dhamana hii kwa uaminifu mkubwa. Ni heshima na wajibu kwangu kuwatumikia wananchi wa Mlangarini . Sasa tumeingia kwenye kazi ya kwenda kushughulikia changamoto za wananchi wetu,” alisema.


Alibainisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo barabara zisizopitika, upungufu wa maji safi na salama, pamoja na uhaba wa umeme katika baadhi ya maeneo.

> “Wananchi wetu wana kiu kubwa ya maendeleo. Wana kero nyingi, baadhi zikiwa zimekita mizizi kwa muda mrefu. Tutafanya kazi kwa nguvu zote kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora zaidi, na nitahakikisha naanzankutekeleza ahadi zangu kwa wakati” aliongeza.


Diwani Mrema amesema kuwa tayari amejiwekea mikakati madhubuti ya kuboresha miundombinu, kusukuma upatikanaji wa maji na kuharakisha usambazaji wa umeme katika maeneo yanayohitaji huduma hiyo.

Aidha, b kushirikiana kikamilifu na madiwani wenzake, viongozi wengine wa serikali na halmashauri pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha rasilimali zinazopatikana zinatumika kwa manufaa ya wananchi.

> “Nitajitahidi kutumia uwezo wangu, maarifa yangu na rasilimali zinazopatikana ili kuhakikisha tunaleta mabadiliko chanya katika halmashauri na jamii kwa ujumla,” Alisema.






Ends..

Post a Comment

0 Comments