SWEDEN YAJITEMGA NA TANZANIA,YASITISHA USHIRIKIANO WA MAENDELEO

By Arushadigital 


SERIKALI ya Sweden imetangaza kusitisha ushirikiano wake na nchi ya Tanzania, kupitia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Sweden nchini imesemea Sweden itasitisha ushirikiano wa maendeleo na Tanzania kufikia tarehe 31 Agosti 2026. 


Kwa sasa ushirikiano wa Sweden na Tanzania utaendelea hadi utakapofika wakati huo.


Aidha, Sweden imesema uamuzi huo unatokana na mabadiliko ya vipaumbele vya sera za kimataifa, na changamoto mpya za kiusalama nchini Tanzania. 


Hata hivyo, Sweden imesema uamuzi huo wa kusitisha uhusiano wake na Tanzania hauhusiani na matukio ya hivi karibuni yaliyotokea nchini Tanzania.


#KitengeUpdates

Post a Comment

0 Comments