AMUUA MKE WAKE BAADA YA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI

By Arushadigital 


JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Chimaguli Majiyangui Samamba (54), mkulima na mkazi wa Ugede-Songambele, kwa tuhuma za kumuua mke wake Moshi Paulo John (47) baada ya ugomvi wa ndoa uliotokana na kuchelewa kurudi nyumbani.


Tukio hilo lilitokea Oktoba 1, 2025, ambapo mtuhumiwa alidaiwa kumpiga mke wake hadi kufariki dunia kisha kumfukia kwenye shimo la choo jirani na nyumba yao.


Majirani waliripoti kutoweka kwa marehemu, na baada ya uchunguzi, Polisi walimkamata mtuhumiwa ambaye alikiri kutenda kosa hilo.


Polisi wamewataka wananchi kutoa taarifa mapema kuhusu matukio ya uhalifu ili kudumisha amani na usalama mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments