AFUNGWA MIEZI SITA KWA KUWAKATA WATOTO WA JIRANI YAKE MASIKIO

Na Arushadigital-BABATI


 MKAZI wa kijiji cha Bermi wilayani Babati mkoani Manyara, Hamis Mfangavu (42) amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani na kulipa fidia ya Sh. milioni moja kwa kosa la kumkata masikio mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka 13 jina limehifadhiwa, akimtuhumu kuiba yai moja.


Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Manyara Martin Masao.


Masao alisema mshtakiwa alimkata masikio mawili Agost 23, mwaka huu mtoto wa kiume jina limehifadhiwa kwa kumtuhumu kuiba yai moja la kuku.


Hakimu alisema mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa mshtakiwa na kuiba yai moja la kuku wakati akitoka alikutana na kaka yake na mshtakiwa ambaye alikuwa amemshikilia na alipofika Mfangavu alisema abaki naye watamalizana.



"Alivyobaki na mtoto huyo alimwingiza chumbani na kumkata masikio mawili kwa wembe na kumpiga kichwani, kifuani na kuumiza kichwa mpaka kikabonyea,"alisema Masao.


Hakimu huyo alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 225 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 200 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023.


Aidha, alisema licha ya mashahidi wengine kuthibitisha mtoto huyo kukatwa masikio na kuumizwa kichwa na kifua ushahidi wa daktari nao ulithibitisha masikio mawili kukatwa na kipande kimoja kukutwa kikining'inia na kusababisha kulazwa Hospitali ya Dareda kwa siku nne na baadaye kupewa Rufani kwenda Hospitali ya Haydom.


"Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na Jamhuri ambao haukuwa na dosari na haukuleta taharuki,"alisema.



Alisema katika utetezi wa Mfangavu hakuungwa mkono na mtu yeyote na hakumwita kaka yake wala mwenyekiti wa Kijiji kufika kumtetea.


Wakili wa Serikali, Esther Malima alisema kosa hilo limefanyika kwa kiwango kikubwa na lina majeraha zaidi ya moja.


Aidha, alisema majeraha aliyoyapata mhanga ni kukatwa masikio na kumsababishia ulemavu na masikio hayataweza kuota tena yametoka moja kwa moja.


Aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa Mfangavu ili iwe fundisho kwa rafiki zake na jamii.


Mzazi wa mtoto huyo, Thomas Herman alipewa nafasi ya kueleza mtoto wake alivyofanyiwa ukatili alisema alikatwa masikio na kumpa uchungu.



Alitaja athari alizozipata mtoto wake kuwa ni kuathirika kisaikolojia, hatakuwa na amani katika jamii na ataishi kwa wasiwasi.


Herman alieleza kuwa hali ya kiafya ya mtoto wake bado siyo nzuri kwa kuwa hakai kwa amani na mwonekano wake ni tofauti na Mungu alivyomuumba.


Alipoulizwa gharama alizotumia kumtibu mtoto wake alisema alitumia zaidi ya Sh.600,000 gharama zingine ni za chakula na kushindwa kufanya kazi za kuajiriwa.


Mzazi huyo aliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa jamii.


Aidha, mahakama ilimpa nafasi mshtakiwa kujitetea ambapo alisema hana cha kuonge

Post a Comment

0 Comments