UZINDUZI WA KISHINDO KAMPENI ZA CCM ARUMERU MAGHARIBI
Na Joseph Ngilisho ARUMERU
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Arumeru Magharibi kinatarajiwa kufanya uzinduzi mkubwa wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dkt. Johannes Lukumay, katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kesho September 4,2025 katika viwanja vya Ngaramtoni.
Akizungumza na vyombo vya habari, mapemam leo September 3,2025 Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM jimboni humo, Nicolaus Sawa, alisema kampeni hizo zitazinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, ambaye atakuwa mgeni rasmi katika tukio hilo kubwa la kisiasa.
Sawa alisema kabla ya hotuba na uzinduzi, kutakuwa na shamrashamra mbalimbali ikiwemo burudani kutoka kwa vikundi vya ngoma za asili na wasanii wa muziki, ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi.
“Tunatarajia mkutano huo wa uzinduzi kuhudhuriwa na zaidi ya wananchi 5,000 kutoka maeneo mbalimbali ya Arumeru Magharibi, sambamba na viongozi wa CCM ngazi ya mkoa na Taifa,” alisema Sawa.
Sawa alisisitiza kuwa chama hicho kimekuwa na muunganiko mkubwa na kesho waliokuwa watia zaidi ya 20 wa ubunge akiwemo mfanyabiashara Maarufu Elias Lukumay watakuwepo kumuunga mkoani Mgombea huyo aliyeteuliwa na chama .
Kwa upande wake, mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lukumay, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tukio hilo, akisema ni fursa muhimu ya kuonesha mshikamano wa wananchi na chama chao.
“Nawakaribisha wananchi wote wa Arumeru Magharibi na maeneo jirani kufika kuanzia saa nne asubuhi viwanja vya Ngaramtoni. Huu ni wakati wa kuonyesha mshikaman0 wetu na kusikiliza dira ya maendeleo tunayoiandaa kwa ajili ya jimbo letu,” alisema Dkt. Lukumay.
Kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho, uzinduzi huo unalenga kutoa dira ya kampeni, kueleza sera na mikakati ya CCM kwa wananchi wa Arumeru Magharibi, pamoja na kumtambulisha rasmi mgombea wao, Dkt. Lukumay, kwa wapiga kura.
Ends...


0 Comments