MAELFU KUTINGA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM ARUMERU MAGHARIBI LEO
Na Joseph Ngilisho-ARUMERU
Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Arumeru Magharibi zinatarajiwa kuzinduliwa kesho September 4,2025 kwa shamrashamra kubwa katika eneo la Ngaramtoni kuanzia saa nane mchana.
Uzinduzi huo utaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, ambaye atamtambulisha rasmi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho, Dkt. Johannes Lukumay.
Maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM kutoka kata mbalimbali za Arumeru Magharibi wanatarajiwa kujitokeza kushuhudia tukio hilo, ambalo linatazamwa kama mwanzo wa safari ya ushindi wa chama hicho katika uchaguzi ujao.
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Dkt. Lukumay amewakaribisha wananchi wote wa Arumeru Magharibi kushiriki kwa wingi, akisisitiza kuwa kampeni zake zitajikita katika ajenda ya maendeleo. “Nawakaribisha wananchi wote wa Arumeru kushiriki uzinduzi huu wa kihistoria. Tutaendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega kusukuma mbele maendeleo ya jimbo letu, hususan katika kilimo, elimu na huduma za jamii,” alisema.
Mkutano huo pia unatarajiwa kupambwa na burudani, nderemo na shamrashamra kutoka kwa vikundi mbalimbali na wafuasi wa chama hicho .
Ends...
0 Comments