KANISA KATOLIKI LACHAFUKWA,LAPIGA MARUFUKU PADRI,MTAWA AU KIONGOZI YOYOTE WA DINI HIYO KUSHIRIKI SIASA

By Arushadigital-Dar Es Salaam

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, ametoa tamko kali la kuwakataza viongozi na watumishi wote wa Kanisa Katoliki kushiriki katika kampeni za kisiasa, akisisitiza kuwa ni kosa kwa mtu aliyejitolea maisha yake kwa Mungu kujiingiza kwenye majukwaa ya siasa.

Akihutubia waumini katika misa ya Jubilei ya Miaka 100 ya Seminari ya Kipalapala mkoani Tabora leo, Askofu Pisa alisema:

> “Mtawa, Padri au kiongozi yeyote wa Kanisa hapaswi kushiriki katika kampeni zozote za siasa. Wala hapaswi kutambulishwa na chama chochote kwa kuvalishwa gwanda lolote la chama cha siasa au kiashiria chochote.”


Aliongeza kuwa kanisa linataka kuendelea kusimama upande wa haki, amani na mshikamano wa kijamii, badala ya kuegemea upande wa chama chochote cha kisiasa:

> “Ni marufuku mapadre, marufuku kwa watawa, marufuku kwa waseminaristi kuonekana kwenye kampeni za siasa. Marufuku kubwa.”


Tamko hilo limekuja siku moja tu baada ya picha kusambaa mitandaoni zikionyesha Masista wa Kituo cha Mtakatifu Benedicto wa Msaada wa Kikristo Afrika (Ndanda) wakihudhuria mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Masasi, Mtwara, wakiwa wameshika machapisho ya kampeni.

Katika hotuba yake, Askofu Pisa pia aliwaonya watawa na mapadre dhidi ya kuvaa mavazi ya vyama vya siasa kama vile kofia, fulana na vitambaa vyenye alama za kisiasa, akisisitiza kwamba heshima ya wito wao inapaswa kulindwa kwa gharama yoyote.

Ends..

Post a Comment

0 Comments