CPA NGUNGATI AVUNJA UKIMYA ,AAHIDI KUMNADI MSHINDANI WAKE DKT LUKUMAY NYUMBA KWA NYUMBA ARUMERU MAGHARIBI

Ngungati Avunja Ukimya, Aahidi Kumnadi Dkt. Lukumay Arumeru Magharibi

Na Joseph Ngilisho, Arumeru


ALIYEKUWA mtia nia wa ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi, CPA Julias Ngungati, amevunja ukimya na kutoa shukrani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo kwa kumpa nafasi ya kushiriki mchakato wa kutia nia.

Ngungati amesema hatua ya chama kumpata mgombea mmoja, Dkt. Johannes Lukumay, imeweka dira mpya ya mshikamano, akisisitiza kwamba sasa makundi yote yamevunjika na wapo pamoja kwa ajili ya ushindi wa chama.

> “Nimetulia na kuamini uamuzi wa chama. Nitapita kata kwa kata, nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa kumpigania kura Dkt. Lukumay, madiwani wetu pamoja na Mama Samia Suluhu Hassan,” alisema.


Alisisitiza kuwa mshikamano wa wanachama ndio silaha ya ushindi na kwamba hana shaka chama hicho kitasonga mbele kwa kishindo katika uchaguzi ujao.






Enda..

Post a Comment

0 Comments