UTEUZI ;AMOS MAKALA RC MPYA ARUSHA , KENANI AONDOLEWA

 By Arushadigital 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi leo August 23 kwa kumteua CPA. Amos Gabriel Makalla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. 


Awali CPA. Makalla alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi na anachukua nafasi ya Kenan Laban Kihongosi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, kabla ya uteuzi huu uapisho wa Mkuu wa Mkoa Mteule utafanyika tarehe 26 Agosti, 2025 saa 05.00 asubuhi, Ikulu Chamwino, Dodoma. 

UTEUZI , KENANI KIHONGOSI.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Kabla ya uteuzi huo, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na CPA Amos Makalla.


Taarifa kuhusu uteuzi huo imetolewa leo, Agosti 23, 2025, na CPA Amos Makalla, wakati akitangaza majina ya wagombea wa nafasi ya Ubunge kupitia CCM


#Arushadigital UPDATES

Post a Comment

0 Comments