MTOTO WA MIAKA MITANO ABAKWA KINYAMA, MTUHUMIWA AKAMATWA
Na Joseph Ngilisho- Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia kijana, Saidi Hussein mwenye umri wa miaka 18 Mkazi wa Mtaa wa Kirika A,kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano, tukio lililozua hasira na simanzi kubwa kwa wakazi wa mtaa huo kata ya Sombetini,Jijini Arusha.
Tukio hilo lilitokea Agosti 5,2025 ambapo inadaiwa majira ya mchana mtuhumiwa alimwita ndani kwake baada ya kumpatia pesa akamtafutie chaji dukani wakati alipokuwa akicheza na wenzake, kisha kumfanyia ukatili huo nyumbani kwa wazazi wake alipokuwa akiishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justine Masejo alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa,na kushikiliwa katika kituo cha Polisi Muriet akieleza kuwa mtoto ameshapelekwa hospitali kwa uchunguzi wa kitabibu na matibabu, huku ripoti ya daktari ikitarajiwa kuwasilishwa kama sehemu ya ushahidi.
>
“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi, askari walifika eneo la tukio haraka na kufanikisha kumkamata mtuhumiwa. Upelelezi unaendelea kabla ya kumfikisha mahakamani,” alisema RPC.
Kauli ya Mtoto !
Akizungumzia tukio hilo mtoto huyo anayesoma chekechea, alisema siku ya tukio akiwa anacheza na wenzake mtuhumiwa alipatia shilingi 1000 ili akamtafutie chenji dukani na aliporudi alimwita ndani na kufunga mlango na kisha kuanza kumvua nguo na kumfanyia tabia mbaya.
Amekuwa akinifanyia mara nyingi na watoto wengine pia amewafanyia tabia mbaya, siku hiyo alinituma nikamletee chenji na niliporudi aliniambia niingie ndani akafunga mlango na kunivua nguo na kuanza kunifanyia tabia mbaya .
Alidai kuwa mara ya kwanza alipomfanyia alienda kumwambia mama yake lakini mama alimjibu kuwa akimfanyia tena aseme ili wampeleke polisi.
Kauli ya Jirani!
Mmoja wa majirani, Magreth Mushi alisema akiwa nyumbani kwake alisikia kelele nyumbani kwa mtoto huyo na alipofika alifahamishwa kuwa mtoto amebakwa na Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Saidi.
"Hili tukio si mara ya kwanza huyu kijana kwanza amefukuzwa shule kwa kukutwa akiwauzia wanafunzi wenzake Bangi pia amekuwa akiwapaka mafuta vijana wadogo wa kiume na kuwafanyia mchezo mbaya tunacgotaka sisi sheria ichukue mkondo wake tumechoka na tabia za huyo kijana na hili sio tukio la kwanza".
Amelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua kali ili kukomesha matukio ya aina hiyo ambayo yamekithiri miongoni mwa vijana wa kiume
>
“Tulipomhoji, akasema Saidi amemfanyia jambo baya. Tulipatwa na hasira sana, lakini tukachagua kutoa taarifa polisi ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema
Kauli ya Baba wa Mtoto
Baba mzazi wa mtoto,Floridi Makauki alisema kitendo hicho kimemuumiza sana na kinavunja ndoto za mtoto wake ,ameliomba jeshi la polisi kuhakikisha mtuhumiwa anachukuliwa hatua stahiki.
>
“Mtoto huyu bado mdogo sana, anahitaji kucheza na kusoma, si kupitia mateso ya namna hii. Naomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema kwa huzuni.
Kauli ya Mama wa Mtuhumiwa
Mama wa mtuhumiwa, Hafsa Husein alisema ameshtushwa na taarifa hizo na kudai hakuwahi kufikiria mwanawe anaweza kuhusika katika kosa hilo.
Alisema siku ya tukio hakuwepo nyumbani alienda kufuata biashara yake ya ndizi sokoni ila baadaye alikuja kupata taarifa kuwa Mwanaye Saidi amembaka mtoto wa jirani.
>
“Siku ya tukio sikuwepo nilichoshuhudia ni maaskari walikuja kumchukua mwanangu Saidi na kuniambia kuwa mwanao amebaka mtoto wa jirani"
Kwa sasa, mtuhumiwa yupo mahabusu na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika. Polisi pia wamewataka wananchi kuongeza ulinzi na uangalizi kwa watoto wadogo ili kuzuia visa vya ukatili wa kijinsia.
Ends...





0 Comments