By Arushadigital-CONGO
Mahakama ya juu nchini DR Congo imeomba kumuhukumu Waziri wa zamani wa Sheria Constant Mutamba kifungo cha miaka 10 na kumnyima haki ya kupiga kura au kushika wadhifa wowote serikalini kwa wakati huo na kurejesha fedha kwenye akaunti ya Serikali.
Mutamba anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa dola za Marekani Milioni 19. Pesa hizo, kwa mujibu wa upande wa mashtaka zilikusudiwa kwa ajili ya ujenzi wa Gereza jipya katika Mji wa Kisangani, kaunti ya Tshopo, kupitia Kampuni ya Zion Construction.
Mwezi Januari 23, 2025, Constant Mutamba alikanusha madai hayo, akieleza kuwa pesa hizo bado ziko kwenye akaunti ya Sayuni Constructions.
Hayo yamekanushwa na Mwendesha Mashtaka, Sylvain Kaluila ambaye alisema Agosti 13 mwaka huu kuwa kampuni ya Zion Construction haipo, bali ni kampuni ambayo iliundwa kutumika kwa shughuli haramu.
#ArushadigitalUpdates
0 Comments