JAJI AJIHUKUMU KESI YA CHADEMA, AKATAA KUJITOA!

By arushadigtal -Dar 


Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, amegoma kujitoa kusikiliza kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


‎‎Kesi hiyo ya madai ya mwaka 2025 iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Zanzibar na wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu huku walalamikiwa wakiwa ni Bodi ya wadhamini waliosajiliwa na Katibu Mkuu wa chama hicho.


‎‎Jaji Mwanga ameisikiliza kesi hiyo tangu Aprili 17, 2025 ilipotajwa kwa mara ya kwanza na kuendelea nayo katika hatua zilizofuata


‎Walalamikaji hwalimwandikia barua  ya kumtaka ajitoe katika kesi hiyo Juni 23, 20255, huku wakimlalamikiwa kuwa na upendeleo kwa upande wa walalamikaji na mgongano wa masilahi na kuwa na mgogoro naye, malalamiko ambayo Jaji Mwanga aliyasikiliza Julai 14, 2025.‎


‎Katika uamuzi wake alioutoa leo Jumatatu, Julai 28, 2025 Jaji Mwanga amezikataa sababu zote zilizotolewa na walalamikiwa akieleza kuwa hazina mashiko.‎ #EastAfricaTV

Post a Comment

0 Comments