INEC YAWANOA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI ARUSHA NA MANYARA,

 Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 


WASIMAMIZI wa uchaguzi 86 kutoka mikoa ya Arusha na Manyara wametakiwa kusimamia viapo vyao na kujitoa kwenye chama chochote cha Kisiasa kwenye kipindi hiki cha uchaguzi ili kuepuka migogoro.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC)  Zakia Abubakary amesema leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo julai 21 hadi 23 kwa waratibu,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi jijini Arusha.

Zakia  alisema watendaji hao wamepewa dhamana ya kusimamia na kuratibu uendeshaji  wa Uchaguzi wa Rais na wabunge pamoja na Madiwani  kwa Tanzania Bara  ambapo ni jukumu kubwa na nyeti kwa mustakabali wa Taifa.

Aliwaomba wasimamie viapo vyao vya kutunza siri na kutokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa katika kipindi chote cha uchaguzi na kutekeleza vizuri majukumu yao.

Aliwataka watendaji hao  kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalumu ya vituo husika na kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na Amani.

Pia aliwataka watendaji hao  kusoma kwa umakini Katiba,Sheria,Kanuni ,miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na tume .

Alisema  Mafunzo kama hayo yanafanyika pia katika   mikoa ya Dar es salaam,Mbeya,Mwanza,Shinyanga,Rukwa na Kusini Pemba.

“Tume iliwaridhia maafisa uchaguzi na maafisa ununuzi kutekeleza kazi za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo uteuzi wenu umezingatia masharti ya kifungu cha sita(1),(2) na 5 na kifungu cha nane ( 1) na( 2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani,”



Zakia aliwasihi wajiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko utoka kwa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi pia wahakikishe wanazingatia ipasavyo katiba ,shera,kanuni ,miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na tume.


Naye Kaimu mkurugenzi wa tume  huru ya Taifa ya uchaguzi INEC, ,Jafari Makupula  alisema lengo ni kuwajengea uelewa na uwezo wa kusimamia shughuli za Uchaguzi kwa watendaji walioteuliwa,”alisema Makupula.

 
Alifafanua kuwa kati yao wanaopatiwa mafunzo hayo wawili ni Waratibu wa uchaguzi Mkoa,Wasimamizi wa Uchaguzi 14,wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo 42,maafisa uchaguzi 14 na maafisa ununuzi 14.




Ends......
 

 

Post a Comment

0 Comments