MTIA NIA CCM AFA KWA AJALI AKIWA KWENYE USAFIRI WA BAJAJ

By arushadigtal-SHINYANGA


Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyekuwa diwani wa kata ya Solwa, Awadh Hafiz pamoja na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika.


Akizungumza kwa simu , Magomi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Ibadakuli, Barabara ya Shinyanga mjini katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga baada ya basi la abiria kuigonga bajaji ya iliyokuwa imebeba abiria,


“Taarifa hiyo ninayo mezani, lakini sipo katika eneo la kazi ninaweza kukupa taarifa zaidi nikifika kazini, ila taarifa niliyonayo ajali imetokea maeneo ya Ibadakuli barabara ya kuelekea Shinyanga mjini,” amesema Kamanda Magoma.


Amesema basi la abiria lilitaka kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari na kwenda kuigonga babaji hiyo.

Amesema kwenye ajali hiyo, watu wawili wamefariki dunia akiwamo aliyekuwa diwani wa Solwa, Awadh Hafiz na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika.


“Lakini pia imejeruhi watu kadhaa ambao idadi haijafahamika, nitakapo fika eneo la tukio nitatoa taarifa kamili ,” amesema Magomi.

Post a Comment

0 Comments