Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MFANYABIASHARA wa sekta ya usafirishaji jijini Arusha ,Patrick Mulokozi amelalamikia Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushindwa kumpa ushirikiano kuweza kupata mali zake ambazo ni mabasi mawili aina ya Costa aliyokuwa amekodisha kwa kampuni ya usafirishaji ya Impala shato inauyofanya biashara ya kusafirisha Abiria na mizigo kwenda nchi jirani ya Kenya.
Patrick ameendelea kupigwa danadana na jeshi la polisi Kwa zaidi ya mwaka mmoja katika kituo Cha polisi Cha kati (Cental Arusha) kunyimwa kufungua mashitaka dhidi ya mtuhumiwa wake.
Alisema alienda kutoa maelezo kituo hicho cha polisi lakini hakuna chochote kilichoendelea ikiwa nipamoja na upelelezi kufanyika na watuhumiwa wake kukamatwa.
Patrick asema kuwa baadhi ya maafisa wa polisi wa NGAZI za juu aliwaomba msaada kusaidia kupata Mali zake na Kila walipotaka ila walikimbama na kigingi kutoka kwa wakubwa zao wa ngazi za juu na kutakiwa kuachana na suala hilo
Patrick anamtuhumu mtu ambaye ni Mdogo Wake na Mbunge wa ambaye kaka yake huyo anatumia nafasi yake ya ubunge kuwapigia simu viongozi ili kumnyima haki yake ya msingi.
Patrick amemwomba Rais Dkt Samia Suluhu Hasan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kumsaidie kupata haki yake kwani hadi sasa hana msaada mwingine
Jitihada za kumpata Mdaiwa huyo ili kujibu tuhuma hizo ikiwa ni pamoja na Kufika Ofisini hazikuzaa matunda mara baada ya kuwaona waandishi wa Habari alikataa kutoa ushirikiano wa kuzungukza chochote juu ya jambo hilo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana ofisini kwake kuzungumzia suala hilo na jitihada zaidi zinaendelea.
Ends..
0 Comments