By arushadigtal.com
Mchungaji wa kanisa la Huduma ya Kristo lililopo mtaa wa FFU kata ya Murieti Jiji Arusha Steven Jacob mwenye umri wa mika 35 anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana asubuhi ya leo Tarehe 16 May 2025 wakati akitoka nyumbani kwake
Wakizungumza mashuhuda na majirani wa eneo hiyo akiwemo baba yake mzazi ambaye ni balozi wa CCM katika shina hilo wamesema waliomteka walifika na gari aina ya Land Cruser lisilokua na namba za usajili ambapo walimkokota kwa nguvu huku mchungaji huyo akipiga kelele za kutekwa lakini haikusaidia na walimtupa kwenye gari kisha kuondoka nae
Siku chache zilizopita Mch Jacob alizungumzia suala la askari waliofariki kwa kupigwa na ajali mereran na kudai kuwa tukio hilo ameonyeshwa na Mungu kuwa ni njia ya kuwakumbusha kutenda haki na kujithmini.
Kwa Njia ya simu tulimtafuta kamanda wa Polisi ili kuthibitisha tukio hilo lakini simu zake hazikupokelewa lakini mwenyekiti wa mtaa amekiri kutokea kwa utekaji katika mtaa wake
0 Comments