WATANZANIA 173 WAREJEA NYUMBANI KUTOKA AFRIKA KUSINI
By Arushadigital-DAR ES SALAAM
Watanzania 173 waliokuwa wakiishi katika Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini wamewasili nchini baada ya kuamua kurejea nyumbani kwa hiari yao.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa ndege maalum kwa ajili ya kuwawezesha raia hao kurejea nchini kwa usalama, kufuatia uamuzi wao wa kuacha kuishi nchini humo na kurejea Tanzania.
Zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Afrika Kusini pamoja na mamlaka husika za nchi hiyo.
Raia hao wamepewa fursa ya kurejea nchini kwa amani, usalama na kwa hiari, huku hatua hiyo ikilenga kuhakikisha wanarejea salama na kuunganishwa tena na familia zao nchini Tanzania.
Urejeshwaji huo unaeleza jitihada za Serikali ya Tanzania za kuhakikisha raia wake walioko nje ya nchi wanapata msaada na ulinzi unaohitajika pale wanapoamua kurejea nyumbani.

إرسال تعليق