Breaking🔥

BREAKING NEWS: NCHIMBI AJIUZULU NAFASI YA MAKAMU WA RAIS

NCHIMBI AJIUZULU NAFASI YA MAKAMU WA RAIS|Na 

c

Joseph Ngilisho

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amejiuzulu nafasi hiyo na kutangaza kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma, akisema uamuzi huo unalenga kumpa Rais Samia Suluhu Hassan nafasi ya kufanya mabadiliko anayoyataka.

Nchimbi amefanya uamuzi huo kupitia barua aliyomwandikia Rais Samia leo, Agosti 25, 2026, akisema atajiuzulu rasmi nafasi hiyo kuanzia Septemba 4, 2026, kwa mujibu wa Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika barua hiyo, Nchimbi alisema Agosti 27, 2025, alimuahidi Rais Samia kuwa angemsaidia yeye na Taifa kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi kwamba siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine wa Rais, angeachia nafasi hiyo.

“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” alisema Nchimbi.

Nchimbi pia alimshukuru Rais Samia na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa imani walionayo kwake, huku akiwashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompa wakati wote wa utumishi wake wa umma.

Alisema pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma, ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.

Ends

Post a Comment

Previous Post Next Post