CCM YAMFUKUZA NCHIMBI UANACHAMA
Na Joseph Ngilisho
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeamua kumfukuza uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya Nchimbi kutangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma.
Nchimbi alitoa tangazo hilo Agosti 25, 2026, kupitia mtandao wa kijamii, akieleza kuwa ameamua kustaafu siasa na utumishi wa umma. Baadaye, Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia uamuzi huo.
Hatua ya CCM kumfukuza uanachama inafuatia uamuzi wake wa kuachana na siasa na utumishi wa umma, huku ikifungua sura mpya katika safari yake ya kisiasa na kiuongozi.
Wakati huo huo Halmashauri Kuu ya CCM Imempitisha Waziri wa Nishati, Deo Ndejembi kuwa Makamu wa Rais
Kufuatia uamuzi huo wa Chama sasa kwa mujibu wa Katiba jina la Ndejembi litapelekwa Bungeni ili kupigiwa kura na Wabunge ya kumuidhinisha rasmi kuwa Makamu wa Rais




Post a Comment