LUKUMAY AITAKA SERIKALI KUVUTA WAWEKEZAJI WA HOTELI ARUMERU MAGHARIBI

 LUKUMAY AITAKA SERIKALI KUVUTA WAWEKEZAJI WA HOTELI ARUMERU 

By Joseph Ngilisho |DODOMA

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lukumay, ameitaka Serikali kuharakisha mikakati ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujenga hoteli za nyota tatu hadi tano katika eneo la Engorika, Kata ya Kiutu, akisema hatua hiyo itasaidia kukuza utalii na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Dkt. Lukumay alitoa ombi hilo bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Waziri mwenye dhamana ya utalii, akieleza kuwa Jimbo la Arumeru Magharibi ni miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa za utalii Kaskazini mwa Tanzania.

Alitaka kufahamu mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wawekezaji wanavutwa kuwekeza katika miundombinu ya malazi ya kisasa, hususan hoteli za nyota tatu na tano, ili kukidhi mahitaji ya watalii na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi katika eneo hilo.

“Jimbo la Arumeru Magharibi ni lango kuu la utalii Kaskazini. Ni mkakati gani wa Serikali wa kuvutia wawekezaji wa kujenga hoteli za nyota tatu au tano katika eneo la Engorika, Kata ya Kiuto, ili kuvutia utalii?” alihoji Dkt. Lukumay.

Katika swali lake, Dkt. Lukumay pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbalimbali anazochukua katika kuimarisha uongozi na maendeleo ya taifa.

Aidha, alimpongeza Naibu Waziri dkt Pius Steven Taifa kwa ziara yake katika Jimbo la Arumeru Magharibi, ambako alitembelea sekta binafsi na kujionea shughuli za uwekezaji, ikiwemo kiwanda kinachohusika na uzalishaji wa bidhaa za afya.

Akijibu swali hilo, Waziri mwenye dhamana ya utalii alisema Serikali imeanza kuweka mkazo katika maeneo ya Arusha yenye fursa za utalii na uwekezaji, huku Arumeru ikitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayolengwa katika mpango huo.

Aidha, alimpongeza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, kwa ziara yake katika Jimbo la Arumeru Magharibi, ambako alitembelea sekta binafsi na kujionea shughuli za uwekezaji, ikiwemo kiwanda kinachohusika na uzalishaji wa bidhaa za afya.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, alisema Serikali imeanza kuweka mkazo katika maeneo ya Arusha yenye fursa za utalii na uwekezaji, huku Arumeru ikitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayolengwa katika mpango huo.

Alisema Serikali inalenga kuvutia wawekezaji kujenga hoteli za kisasa, zikiwemo za kiwango cha nyota tano, kwa lengo la kuongeza uwezo wa Tanzania kuhudumia watalii wanaofika nchini.

“Katika vipaumbele na mikakati yetu ya kuvutia wawekezaji kwenye suala la utalii, eneo la Arumeru ni moja ya maeneo ambayo tumeanza kuyafanyia kazi kuhakikisha tunavutia wawekezaji wa kujenga hoteli za kisasa, hoteli za nyota tano na hoteli za kitalii,” alisema.

Waziri huyo alisema uwekezaji huo hautalenga kuimarisha sekta ya utalii pekee, bali pia utasaidia kukuza uchumi wa Arumeru na kuongeza kipato kwa wananchi kupitia ajira, biashara na huduma mbalimbali zitakazohusishwa na sekta hiyo.

“Katika vipaumbele na mikakati yetu ya kuvutia wawekezaji kwenye suala la utalii, eneo la Arumeru ni moja ya maeneo ambayo tumeanza kuyafanyia kazi kuhakikisha tunavutia wawekezaji wa kujenga hoteli za kisasa, hoteli za nyota tano na hoteli za kitalii,” alisema Dkt. Chaya.

Dkt. Chaya alisema uwekezaji huo hautalenga kuimarisha sekta ya utalii pekee, bali pia utasaidia kukuza uchumi wa Arumeru na kuongeza kipato kwa wananchi kupitia ajira, biashara na huduma mbalimbali zitakazohusishwa na sekta hiyo.

Pia alimpongeza Dkt. Lukumay kwa juhudi za kushirikisha sekta binafsi katika maendeleo ya jimbo hilo, akisema ziara yake ya kutembelea Arumeru Magharibi imempa fursa ya kujionea uwekezaji unaoendelea na fursa zilizopo.

“Arumeru Magharibi ni sehemu ya Mkoa wa Arusha na tunatambua Arusha ni mkoa ambao tunauitegemea sana kwa utalii,” alisema Waziri huyo.

“Arumeru Magharibi ni sehemu ya Mkoa wa Arusha na tunatambua Arusha ni mkoa ambao tunauitegemea sana kwa utalii,” alisema Dkt. Chaya.

Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Dkt. Lukumay pamoja na wadau wengine kuhakikisha fursa za uwekezaji katika utalii zinatambuliwa na kutumika kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Hatua hiyo inatajwa kuwa muhimu kwa Arumeru Magharibi, eneo ambalo linaendelea kutazamwa kama sehemu yenye uwezo wa kuongeza bidhaa za utalii Kaskazini, huku uwekezaji katika hoteli na huduma za kitalii ukitarajiwa kuongeza muda wa watalii kukaa katika maeneo hayo na kuchochea mnyororo mpana wa shughuli za kiuchumi.

Ends. 

Post a Comment

أحدث أقدم