WAZIRI WA ULINZI AUAWA KWA RISASI

By Arushadigital 


Waziri wa Ulinzi wa Mali, Sadio Camara, ameripotiwa kuuawa katika shambulio lililolenga makazi yake ndani ya kambi ya kijeshi ya Kati, nje ya mji mkuu Bamako.


Kwa mujibu wa redio ya Ufaransa RFI, shambulio hilo lilitokea Jumamosi na linahusishwa na kundi la JNIM lenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda. Ripoti hiyo imetolewa leo Jumapili, huku mamlaka za Mali zikiwa bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.


Tukio hilo linakuja wakati hali ya usalama nchini Mali ikiendelea kuwa tete, huku makundi ya wenye silaha yakiripotiwa kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Post a Comment

0 Comments