WATUHUNIWA WANNE WEZI LA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA AMBLENCE WAKIWEMO WAKAZI WA ARUSHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

WATU WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA GARI LA WAGONJWA MUSOMA, WALIBADILI KUWA LA UTALII

Na Arushadigital — Musoma

Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma wakikabiliwa na tuhuma nzito za wizi wa gari la kubeba wagonjwa la Manispaa ya Musoma, ambalo inadaiwa baadaye lilifanyiwa mabadiliko na kuanza kutumika kama gari la biashara ya kubeba watalii.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani Februari 13, 2026 na kusomewa mashtaka matatu, likiwemo la uhujumu uchumi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 26, 2026 baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi bado haujakamilika.


Akisoma majina ya washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Hadija Masala, Wakili wa Serikali Michael Kayombo aliwataja kuwa ni Goodluck Chacha (26), dereva na mkazi wa Tarime mkoani Mara; Karume Kihedu (26), fundi mekanika mkazi wa Arusha; pamoja na Saidi Ramadhani (39) na Elias Joakim (53), wote mafundi mekanika na wakazi wa Arusha.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika na mpango wa kuiba gari hilo la huduma za afya linalomilikiwa na Manispaa ya Musoma, kisha kulibadilisha muonekano na matumizi yake ili kuficha utambulisho wake wa awali kabla ya kuingizwa kwenye shughuli za kibiashara za utalii.

Tukio hilo limeibua mjadala mpana miongoni mwa wakazi wa Musoma na wadau wa sekta ya afya kuhusu usalama wa mali za umma, hususan magari ya dharura yanayotegemewa kuokoa maisha ya wananchi.

Upande wa mashtaka umeiomba Mahakama kuendelea kuwashikilia washtakiwa hadi upelelezi utakapokamilika, huku Mahakama ikiahirisha shauri hilo kwa hatua zaidi za kisheria.



Ends .

Post a Comment

0 Comments