WASHTAKIWA 79 KATI YA 191 WA UHAINI ARUSHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI MAMIA WAFURUKA KUONA NDUGU ZAO-WALIOSUBIRI KUACHIWA HURU WAGONGA MWAMBA,SOMA NDANI MAJINA YA WATUHUMIWA NDANI

WASHTAKIWA 79 WA MAKOSA YA UHANI ARUSHA WAPELEKWA MAHAKAMANI — UPELELEZI BADO WAGONGA MWAMBA

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Novemba 19,2025 ilikumbwa na pilikapilika nzito baada ya washtakiwa 79, kati ya 191, wanaodaiwa kuhusika katika makosa ya kula njama na kufanya vitendo vya uhaini, kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa kwa mashauri yao.


Hali ya taharuki ilitanda nje ya mahakama kutokana na idadi kubwa ya ndugu, jamaa na wanaharakati waliokusanyika wakitaka kufahamu hatima ya wapendwa wao. Ndani ya chumba cha mahakama, utulivu ulitawala huku maafisa magereza na askari wakiwa katika ulinzi mkali.


Mashauri hayo matatu yalitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Erasto Phill, ambapo Wakili wa Serikali Gilbart Msuya aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hizo bado haujakamilika kutokana na wingi wa washtakiwa, shughuli za uchunguzi 

TANGAZO!PATA OFFER KUTOKA KAMPUNI YA UTALII YA RIBRIS SAFARIS



Kesi ya Kwanza (Na. 26512/2025): Washtakiwa 54

Katika shauri hili, linalowahusu washtakiwa 54 wakiongozwa na Aidani Lyimo, Wakili Msuya alisema limefikishwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa pekee kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika. Alifafanua kuwa miongoni mwa maeneo yanayohitaji muda zaidi ni uchambuzi wakina uweze kufanyika.

Kesi ya Pili (Na. 26514/2025): Washtakiwa 21


Shauri hili likiwa na washtakiwa 21 wakiongozwa na Antony Chuwa, nalo liliwasilishwa kwa utaratibu wa kutajwa. Upande wa Jamhuri uliomba muda zaidi kukamilisha upelelezi ambao umedaiwa uchakataji wa washtakiwa unaendelea


Kesi ya Tatu (Na. 26534/2025): Washtakiwa 5


Katika kesi hii yenye washtakiwa watano, upande wa mashtaka uliiomba mahakama muda mwingine wa kukamilisha upelelezi.

Jopo la mawakili wa utetezi likiongozwa na Hamisi Mkindi liliomba kupatiwa hati ya mashtaka ili kuanza maandalizi ya kesi. Aidha, waliitaka mahakama kufuatilia utekelezaji wa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyewahi kuelekeza kuwa wale ambao hawakuhusika na makosa hayo waachiliwe mara upelelezi unapobainisha kutokuwa na ushahidi dhidi yao.


Mkindi alisema: “Ni muhimu haki itendeke kwa wakati. Kauli ya Mheshimiwa Rais ilikuwa wazi—wasiohusika waachiwe. Tunaomba mahakama isimamie hilo.”


Kauli hiyo ilizua gumzo miongoni mwa ndugu waliokuwa wamejaa nje ya chumba cha Mahakama, ambao walionekana kufarijika na hatua hiyo huku wakisubiri kwa shauku kitakachofuata.


Hakimu Phill aliutaka upande wa Jamhuri kuharakisha upelelezi ili kuwabaini mapema wale wasioguswa na tuhuma hizo. Aliagiza pia hati za mashtaka kukabidhiwe kwa utetezi bila kuchelewa ili kuhakikisha haki inatendeka bila urasimu.

Mahakama iliahirisha mashauri yote hadi Desemba 3, 2025, saa tatu asubuhi, yatakaporejea kwa hatua ya kutajwa upya. Hadi wakati huo, washtakiwa wote wataendelea kusalia mahabusu kutokana na kosa la uhaini ambalo halina dhamana kisheria

Nje ya Mahakama

Nje ya Mahakama wakili wa Utetezi Hamisi Mkindi na wenzake,Ally Mhyellah na Sheck Mfinanga aliongea na ndugu wa washtakiwa na kuwasomea majina ya ndugu zao waliofikishwa mahakamani hapo.

Alisema Washtakiwa wa kundi la kwanza  walikuwa 53 wakiongozwa na Aidani Lyimo ,Wilson  Ndiogi,Gidioni Raphael ,Said Ally Mwinjuma na Frank Mbise, 

Wingine ni Elibariki Damas, Gidioni Raphael, Arnold Athanas,Omari Idy ,Elisha Marick,Charles Richard , Benson Maico,Esau Lukumay, Robert Paulo,Inosent Leon,Olais Mollel, Brighton Kaaya, Denis Kaaya , Hussein Iddy , Ramadhani Hasan na Nelson Thobias.

Wengine ni Ramadhani Hamis,Fabian Raphael, Jackson Mbise, Athumani Hamis Mkoma,John Shayo, Emmanueli Mbise, Timotheo Mafie, Nickson Mbise, Immanuel Shila, Jasper Shoo, Bonface Abel,James Nasari, Abubakary Hamidu,Maico Minja.

Wengine ninElijahson Leopard, Erick Emannuel, Frederick Palangyo,Aman Good luck Meela, Visent Menas Msami,Hafidhi Yusuphu, Nehemiah Good luck, Bon Ventura Husein, Gerard Simon mbise ,Tumain Willbrod,Elineheri kundaheri ,Alex Joachim Emmanueli, God living Elibariki Ndosi,Julias Kilusu,Daniel Zabron,Haruna Hasani na Erick Emannuel.

Hata hivyo baadhi ya wazazi walilalamikia uwepo wa watoto wao wadogo ndani ya gereza wakiwemo wanafunzi ambao walipaswa kufanya mtihani wa kidato cha Pili ulioanza.


nds..

Post a Comment

0 Comments