Na Joseph Ngilisho, Arusha
BALOZI Meja Jenerali Wilbert Ibuge, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), amesema ziara ya maafisa waandamizi kutoka nchi 17 barani Afrika na nje ya bara inayoendelea jijini Arusha inalenga kujifunza kwa vitendo namna sekta ya utalii na uchumi zinavyounganishwa na masuala ya usalama wa taifa.
Akizungumza leo Novemba 10,2025 baada ya kupokea ugeni huo mzito wa maafisa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nchi 17 za Afrika na nje ya Afrika , mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, amewahakikishia usalama na utulivu siku zote tano wawapo mkoani hapa,katika kushiriki mafunzo ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College – NDC).
>
“Arusha ni kitovu cha utalii na uchumi wa Kanda ya Kaskazini. Nawakaribisha mjisikie mko nyumbani. Mkoani kwetu kuna usalama wa kutosha kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama,” alisema CPA Makalla.
"Ni kawaida kila mwaka chuo chetu kutembea Arusha hususani ndio kitovu cha taifa kwenye sekta ya utalii lengo ni kuelewa kitovu cha utalii kinaendeleaje na mikakati yake"
Katika programu hiyo inayojulikana kama “Tentative Programme for Economy in Tourism”, washiriki wanatarajiwa kutembelea taasisi na vivutio muhimu vya utalii ikiwemo Makao Makuu ya TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na maeneo ya kihistoria na kitamaduni ndani ya Jiji la Arusha.
Kwa mujibu wa Mkuu wa NDC, Meja Jenerali Ibuge, mafunzo hayo yanawapa washiriki fursa ya kujifunza uhusiano kati ya utalii, uchumi na usalama wa kikanda, sambamba na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma miongoni mwa nchi wanachama.
>
“Tunataka washiriki wetu waone namna Tanzania inavyotumia rasilimali zake za utalii kwa manufaa ya kiuchumi bila kuhatarisha usalama wa taifa. Arusha ni mfano bora wa uhusiano huo,” alisema Meja Jenerali Ibuge.
Mafunzo hayo ya NDC ni sehemu ya mfululizo wa programu za kimkakati zinazolenga kukuza ushirikiano wa kikanda katika masuala ya ulinzi, usalama na maendeleo endelevu.
-ends..


















0 Comments