BAA YA PICNIC HAIHUSIKI NA TUKIO LA KIFO CHA ASKARI POLISI KAMA ILIVYORIPOTIWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Na Arushadigital — Arusha
Uongozi wa Picnic Bar iliyopo eneo la Kaloleni jijini Arusha umetolea ufafanuzi taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikidai kuwa tukio la kuuawa kwa askari polisi aliyetajwa kwa jina la Omari Mnandi lilitokea katika eneo la baa hiyo.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, uongozi wa Picnic Bar umekanusha vikali taarifa hizo na kubainisha kuwa tukio hilo halikutokea katika eneo la baa hiyo, bali lilitokea katika bar ya Simaloi ambayo pia ipo eneo la Kaloleni jijini Arusha.
> “Tunapenda kueka wazi kwa wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba tukio hilo la kusikitisha halikutokea katika baa yetu. Picnic Bar haikuhusishwa kwa namna yoyote na tukio hilo. Samahani kwa usumbufu na taharuki iliyosababishwa na taarifa hizo zisizo sahihi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Uongozi wa baa hiyo pia umewataka wananchi na wadau wa vyombo vya habari kuwa makini katika utoaji na usambazaji wa taarifa, ili kuepuka kuharibu taswira ya taasisi au biashara zinazohusishwa kimakosa na matukio.
> “Tunaendelea kutoa huduma zetu kama kawaida katika mazingira tulivu na salama, na tunawakaribisha wateja wote bila wasiwasi,” imeongeza taarifa hiyo.
Mwisho.
-ends


0 Comments