TEMBO ZAIDI YA 100 WASOGEZWA BURIGI-CHATO, WANANCHI WAPUMUA

 

TEMBO ZAIDI YA 100 WASOGEZWA BURIGI-CHATO, WANANCHI WAPUMUA

Na Joseph Ngilisho- CHATO

CHATO, Oktoba 4, 2025 – Zoezi la kuswaga makundi mawili ya tembo kutoka maeneo ya makazi ya wananchi na kuwapeleka katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato limeendelea leo, likihusisha zaidi ya tembo 100.

Uhamishaji huo umelenga kuondoa migongano kati ya binadamu na wanyamapori, hali ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi waliokuwa wakivamiwa na tembo katika mashamba na makazi yao.





Kwa mujibu wa mamlaka husika, hatua hiyo imeleta matumaini mapya ya usalama baada ya wananchi wengi kuathirika kwa uharibifu wa mali, mazao, na wakati mwingine hata kupoteza maisha kutokana na mashambulizi ya wanyamapori hao wakubwa.

Zoezi hilo ni mwendelezo wa jitihada za serikali na taasisi za uhifadhi kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na wanyamapori bila migongano, huku tembo wakipata makazi salama ndani ya hifadhi za taifa.

Wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema wamepumua kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu wa hofu na wasiwasi, wakieleza kuwa sasa wana matumaini ya kuendesha shughuli zao za kilimo na makazi bila bughudha.

Ends...

Post a Comment

0 Comments