Na Arushadigital
Idara ya Uhamiaji Nchini imesema imelazimika kuwaondosha Nchini Tanzania Raia wawili wa kigeni ambao ni Dkt. Brinkel Stefanie mwenye hati ya kusafiria ya Ujerumani namba C475MMNGL na Catherine Janel Almquist Kinokfu mwenye hati ya kusafiria ya Marekani namba A80321764 baada ya kubainika kuwa wamekiuka masharti ya viza zao za matembezi.
Kufuatia tukio hilo, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Jijini Dodoma, SSI. Paul J. Mselle ametoa wito kwa Raia wa kigeni wanaoingia na kuishi Nchini kwa madhumuni mbalimbali kuzingatia matakwa yaliyoainishwa katika viza au vibali vyao kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji sura 54 pamoja na kanuni zake ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza pindi wanapokiuka sheria.
Ends .

0 Comments