By Arushadigital -RUVUMA
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limesema Padri Camilius Nikata aliyekuwa akitafutwa tangu Oktoba 8, mwaka huu amepatikana akiwa hai, licha ya kuonekana dhoofu kutokana na kilichadaiwa kuwa njaa kwakuwa alikuwa akishindia karanga na maji.
Kiondozi huyo wa kidini ni padri wa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Radio Maria Tanzania kwa zaidi ya miaka 20 na mpaka anatoweka alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Maiko Chilya amesema kuwa Padri Nikata amepatikana katika mashamba ya kijiji cha Mawa. Na kwamba awali alikuwa anajiandaa kwa safari kwa kutumia usafiri wa basi kuelekea Mwanza Oktoba 8, na alikata tiketi Oktoba 7 na siku hiyo jioni hakuonekana tena.
Pia Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Damiani Denis Dallu ametangaza mkesha wa maombi ambako Jumatatu Oktoba 13 waumini parokia ya Songea walikuwa na mkesha kumwombea Padri Nikata apatikane akiwa hai.

0 Comments