12 WAKAMATWA VURUGU NA MAANDAMANO SIRARI,HECHE AKAMATWA MAHAKAMANI

 By Arushadigital 


Jeshi la Polisi limethibitisha kuwakamata watu 12 ambao ni waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda katika Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya mkoani Mara baada ya kufanya fujo na kufunga barabara katika mji wa Sirari jana Oktoba 21, 2025.


Taarifa ya Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya imesema kuwa chanzo cha fujo hicho kimetokana na kukamatwa kwa vijana wawili (2) mnamo majira ya saa 11: 30 jioni kwa mujibu wa sheria na kuwafikisha katika Kituo cha Polisi Tarime.


“Baada ya watuhumiwa hao kufikishwa kituoni, vijana wa bodaboda waliopewa taarifa potofu na ambao walishuhudia watuhumiwa hao kufikishwa kituoni walirudi eneo la mji wa Sirari na bila halali yoyote na kwa makusudi wakajaribu kufanya fujo na kufunga barabara,” taarifa hiyo imesema.


Jeshi la polisi liliwatawanya vijana hao na kufanikiwa kuwatia nguvuni bvijana hao 12 na watachukuliwa hatua pindi taratibu za kisheria zitakapokamilika.


Kufuatia tukio hilo, Jeshi la polisi Tarime Rorya limewataka wenye tabia za kufanya fujo kuacha mara moja kwani watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.


Wakati huo huo makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Heche amekamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi muda mfupi baada ya kuwasili Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam.


Camera  zimenasa tukio hilo ambaapo Askari Polisi waliingia katika gari ambalo ndani yake alikuwepo Heche na kisha kuondoka naye.


Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema hawajafahashwa sababu za kukamatwa kwa Heche, AyoTV inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kutoka Jeshi la Polisi ili kufahamu sababu za kukamatwa kwake. 

Ends


Post a Comment

0 Comments