Dkt. Johannes Lembulung Lukumay: Mbunge Mtarajiwa wa Arumeru Magharibi Anayeishi kwa Matendo, Siyo Maneno
Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
KATIKA uwanja wa siasa za Tanzania, jina la Dkt. Johannes Lembulung Lukumay limeibuka kama mfano wa mwanachama mtiifu na kiongozi asiye na mashaka katika misingi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Safari yake imejaa ushuhuda wa uaminifu, nidhamu na mchango wa hali ya juu kwa chama na kwa wananchi wa Arumeru Magharibi.
Mwanzo wa Safari ya Kisiasa
Dkt. Lembulung alianza safari yake ya kisiasa akiwa kijana mdogo, akijitosa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Tangu ujana wake, alikuwa akihusiana kikamilifu na shughuli za chama, akishiriki kampeni, semina na vikao mbalimbali. Hata alipokuwa chuoni, alibaki mwanachama “kindakindaki” – mtu aliyekuwa tayari kutumia muda na rasilimali zake binafsi kuhamasisha wenzake kuunga mkono CCM.
Moyo wake wa kujitolea ulimjenga kama kiongozi mwenye maono, nidhamu na msimamo thabiti, sifa ambazo zimeendelea kumtambulisha hadi leo.
Nafasi za Uongozi Ndani ya Chama
Kadiri alivyokua, alipewa nafasi nyingi za uongozi ndani ya CCM na jumuiya zake. Amewahi kushika nafasi katika UVCCM, Umoja wa Wazazi na Halmashauri za chama kuanzia ngazi ya kata, wilaya hadi mkoa.
Kwa sasa, Dkt. Lembulung ni:
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Arumeru
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha
Mlezi katika jumuiya na kata nyingi za chama
Uwezo wake wa kujenga hoja na kuunganisha wanachama umem
IKIWA imebaki takribani mwezi mmoja na siku Kadhaa kabla hajavaa joho la ubunge, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay anayegombea katika jimbo la Arumeru Magharibi, jimbo lisilo na upinzani ,tayari ameacha alama kwa Watanzania.
Ni simulizi ya kiongozi asiyependa makelele ya majukwaani, bali anayejipambanua kwa matendo yanayoleta matumaini mapya kwa jamii.
Safari ya Berlin Yazaa Fursa
Mwishoni mwa mwaka 2024, akiwa katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani, Dkt. Lembulung alikutana na Dr. Ursula Süßbier, Mkurugenzi wa taasisi ya afya ya meno DENTOGLOBAL. Katika mazungumzo yao, walijadili changamoto kubwa inayolikabili taifa hilo – upungufu wa madaktari wa meno na wasaidizi wa afya ya kinywa.
Kutoka hapo ndipo ikazaliwa fursa ya kipekee kwa Watanzania. Makubaliano yao yalilenga kuandaa vijana wa Kitanzania, kuwashindanisha kwa sifa maalum, na kisha kuwapeleka kufanya kazi katika kliniki na taasisi mbalimbali nchini Ujerumani.
Zaidi ya ajira 100 mpya zinatarajiwa kupitia mpango huu.
Watanzania Kufaidi Ajira na Maarifa
Kwa upande wa Tanzania, Dkt. Lembulung alihakikisha Wizara ya Afya na taasisi husika zinahusishwa moja kwa moja katika uratibu wa mchakato huu. Kwa upande wake, Dr. Ursula kupitia DENTOGLOBAL ameahidi kusaidia vijana hao kwa maandalizi ya makazi, mafunzo ya lugha, utamaduni na stadi za kitaaluma mara watakapowasili Berlin.
Faida ya mpango huu si ajira pekee. Wataalamu hao wakirejea nchini watakuwa wamebeba maarifa mapya, teknolojia ya kisasa na uzoefu wa kimataifa utakaoinua sekta ya afya Tanzania.
Daraja la Ushirikiano wa Kimataifa
Hadithi hii ni zaidi ya makubaliano ya kikazi. Ni daraja jipya la ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani – daraja linaloibua ajira, taaluma na matumaini kwa maelfu ya Watanzania. Ni fursa ya familia nyingi kupata faraja kupitia kipato, elimu na nafasi ya kushiriki katika maendeleo ya taifa.
Kauli za Wananchi
Wananchi wa Arumeru Magharibi wamesema Dkt. Lembulung ni kiongozi mwenye dira na anayejali zaidi maslahi ya jamii.
"Kiongozi huyu si mtu wa maneno mengi, kila hatua yake imejaa matunda. Tunamwona kama mtu sahihi wa kutupeleka mbele," alisema Bi. Regina Kaaya, mama wa watoto wawili kutoka Usa-River.
Kwa upande wake, kijana Musa Gabriel, ambaye anamaliza masomo ya uuguzi, alisema: "Mpango huu wa ajira na mafunzo Ujerumani umetupa matumaini sisi vijana. Tukipata nafasi kama hizi, tutarudi na maarifa makubwa kwa taifa letu. Huyu ndiye mbunge tunayemhitaji."
Naye mzee wa kijiji cha Poli, Mzee Lazaro Ndemu, aliongeza: "Tangu zamani tulitaka kiongozi ambaye hatuoni tu kwenye mikutano, bali tunamuona kwenye vitendo. Dkt. Lembulung anaonesha mfano wa uongozi wa kweli."
Uongozi wa Kimatendo
Kwa msingi huu, Dkt. Lembulung amejipambanua kuwa kiongozi wa vitendo. Badala ya kutumia muda mwingi kutoa maneno makali ya kisiasa, anajieleza kwa hatua zinazobadilisha maisha ya watu.
Kwa wananchi wa Arumeru Magharibi, jina la Dkt. Johannes Lembulung Lukumay linabeba taswira ya mbunge mtarajiwa mwenye dira ya maendeleo, anayejali jamii na mwenye uwezo wa kugeuza changamoto kuwa fursa.
Huyu ndiye kiongozi ambaye Arumeru Magharibi inamtarajia – mbunge asiye na makelele, bali mwenye matendo makubwa.
Ends
0 Comments