MACHAFUKO NEPAL JESHI LAZUIA RAIA KUTOKA NJE ,RAIA WALIA NA UFISADI SERIKALINI

 By Arushadigital


 Jeshi la Nepal limeshika doria katika mitaa ya mji mkuu Kathmandu, baada ya taifa hilo la kukabiliwa na machafuko mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa ambapo Maandamano ya kupinga ufisadi serikalini yaligeuka na kuwa vurugu kuanzia siku ya Jumanne.


Waziri mkuu wa Nepal amejiuzulu huku nyumba za wanasiasa zikiharibiwa, majengo ya serikali yakichomwa moto na bunge likivamiwa na kuchomwa moto.


Makundi ya vijana nchini humo maarufu "Gen Z" yanayoongoza maandamano hayo yamejitenga na uharibifu huo, yakisema maandamano hayo "yalitekwa nyara na watu waliohisi wamepata "fursa" ya kufanya uharibifu.


Jeshi la Nepal limetoa amri ya kutotoka nje kote nchini humo hadi Alhamisi asubuhi, likionya kuwa hatua kali itachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na ghasia hizo zilizosababisha uharibifu Mkubwa.


....

Post a Comment

0 Comments