LISU ATAJA VIGOGO WA SERIKALI MASHAHIDI KATIKA KESI YAKE YUMO RAIS SAMIA

By arushadigital-Dar 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya Uhaini inayoendelea Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam, amewaanika Mashahidi wa upande wake katika kesi hiyo.


Akiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Lissu amesema: “Shahidi wangu wa 1 ni Samia Suluhu Hassan. Huyu anapatikana Ikulu ya Kivukoni. Akikosekana anapatikana Ikulu ya Dodoma.”


“Shahidi wangu wa 2 anaitwa Philip Isdor Mpango. Huyu anapatikana ofisi ya makamu wa Rais, mji wa Serikali Dodoma. Shahidi wangu wa 3 anaitwa Kassim Majaliwa Kassim. Huyu anapatikana ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.


Shahidi wangu wa 4 anaitwa Inspector General of Police (IGP), Camillus Wambura. Huyu anapatikana makao makuu ya polisi Dodoma. Shahidi wangu wa 5 anaitwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhani Kingai. Huyu anapatikana ofisi ya makao ya polisi Dodoma.


Shahidi wa 6 ni Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Huyu simfahamu jina. Lakini anapatikana yalipo makao makuu ya usalama wa Taifa. Shahidi wangu wa 7 anaitwa Kamishna wa Polisi (DCP) Ramadhani Ng'anzi. Huyu anapatikana makao makuu ya polisi Dodoma.


Shahidi wangu wa 8 anaitwa Agather Atuhaire. Huyu yupo Kampala, Uganda. Yule aliyetekwa nyara na kuteswa na kwenda kutupwa mpakani. Shahidi wangu wa 9 ni Boniface Mwangi. Huyu yupo Nairobi, Kenya. Huyu alitekwa nyara, akateswa na kwenda kutupwa mpakani Horohoro.


Shahidi wangu 10 atakuwa John Marwa. Huyu ni Mkurugenzi wa Jambo TV. Shahidi wangu wa 11 atakuwa Amani Sam Golugwa. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA. Huyu anajua mkutano huo uliitishwaje.


Shahidi wangu wa 12 ni John Wegesa Heche. Huyu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. Anajua nilikuwa wapi kipindi hicho. Shahidi wangu wa 13 atakuwa John John Mnyika. Huyu ni Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ofisi yake ni Makao Mkuu ya CHADEMA. Shahidi wangu wa 14 atakuwa Dr. Willy Munyoki Mutunga anapatikana Nairobi, Kenya.


Shahidi wangu wa 15 atakuwa ni Martha Wangari Karua. Huyu anapatikana Nairobi, Kenya. Naomba nihifadhi haki yangu ya kuwaita mashahidi wa ziada kama hawa hawatatosha"


#Arushadigital#

Post a Comment

0 Comments