By arushadigital-Dar
Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeanza kusikilizwa leo Septemba 8, 2025 katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Kesi hiyo inasikilizwa mbele jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru.
Shauri hilo lilipangwa kuanza kwa usikilizwaji wa awali lakini jambo hilo lilishindikana baada ya Lissu kuweka mapingamizi mawili.
Pingamizi la kwanza ni uhalali wa Mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo kwa kile alichodai kuwa kuna masuala mengi yalikosewa katika Mahakama ya Kisutu. Aidha, Lissu alihoji unalali wa mashtaka anayotuhumiwa nayo.
Awali, kwa mujibu wa sheria, wakili wa Serikali Neema Saruni aliteuliwa na Mahakama kwenda kuwa wakili wa Lissu kutokana na asili ya kosa analokabiliwa nalo.
Hata hivyo, wakili huyo aliiambia Mahakama kuwa mteja wake amesema atajitetea mwenyewe kauli ambayo hata Lissu aliithibiitishia Mahakama.
Akizungumza kuhusu mawakili, Lissu amesema kama ilivyokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mahakamani hapo atajitetea mwenyewe kwani kosa analotuhumiwa ni kubwa na anapaswa kupambana mwenyewe.
Akaongeza kuwa, amekuwa mwanasheria na wakili kwa miaka zaidi ya 20 sasa na hivyo Mahakama isiwe na wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kujitetea na anaishukuru kwa kumpa wakili.
Hata hivyo, wakati Lissu anaanza kujitetea kuhusu mapingamizi yake aliyoweka Mahakamani hapo, ilibainika kuwa nyaraka kutoka Mahakama ya Kisutu aliyopewa na ile waliyo nayo mawakili wa serikali pamoja na jaji ni tofauti.
Kutokana na utofauti huo, Jaji alielekeza kuwa kesi ihiyo iahirishwe kwa muda ili apate muda wa kuipitia upya nyaraka ambayo hana ili aweze kuendelea na hoja zake vizuri.
Lissu anakabiliwa na shitaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Anadaiwa kuwa akiwa raia wa Tanzania, kwa nia ya uchochezi alishawishi umma kuzuia kufanyia kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku akitamka na kuandika maneno ya kumshinikiza kiongozi Mkuu wa Serikali ya Tanzania

0 Comments