KATIBU WA ITIKADI, SIASA NA UENEZI CCM ATAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UJIO WA RAIS SAMIA MKOANI ARUSHA

 KATIBU WA ITIKADI, SIASA NA UENEZI CCM ATAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UJIO WA RAIS SAMIA MKOANI ARUSHA

Na Joseph Ngilisho– Arusha



Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Saipulaini Remsey, anatarajiwa kufanya mkutano maalum na vyombo vya habari mnamo Septemba 30, 2025, katika Viwanja vya Kilombero, jijini Arusha, kuzungumzia maandalizi ya ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ataanza ziara yake mkoani humo kuanzia Oktoba 1 hadi 2, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama, mkutano huo unatarajiwa kuvuta hisia kubwa kwani Katibu Remsey atafafanua kwa kina ratiba ya ziara ya Rais Samia, ajenda kuu za kampeni za chama hicho, pamoja na maandalizi ya mapokezi makubwa yanayoratibiwa na CCM mkoani Arusha.

Ziara ya Rais Samia imetajwa kuwa ni sehemu ya kampeni za kitaifa za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo atakutana na wananchi wa Arusha, kuzungumza juu ya dira ya maendeleo ya awamu ijayo, na kuhimiza mshikamano, amani na mshikikano wa kitaifa.

Akizungumzia maandalizi hayo, Katibu Saipulaini Remsey alisema: “Wananchi wa Arusha wajiandae kumpokea kwa shangwe mama yetu, Rais Samia Suluhu Hassan. Ziara hii si ya kawaida bali ni ya kihistoria, itakayodhihirisha mshikamano wetu na dhamira ya CCM kuendeleza maendeleo ya Watanzania wote.”

Mapokezi hayo yameandaliwa kuwa ya kipekee, yakipambwa na burudani za muziki wa kizazi kipya, ngoma za asili, na gwaride maalum la vijana wa chama, ishara ya mshikamano na dhamira ya CCM kuendeleza maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

Ends..

Post a Comment

0 Comments