SIKU CHACHE BAADA YA NDUGAI KUZIKWA MAKADA 24 COM WANALITAKA JIMBO LA KONGWA

By Arushadigital -DODOMA 


Wagombea 24 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge mstaafu na Mbunge wa jimbo hilo, Hayati Job Ndugai. Tukio hilo limefanyika jana, Agosti 12, 2025.


Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa CCM kuanza upya mchakato wa kujaza nafasi hiyo, baada ya Hayati Ndugai kuibuka mshindi kwenye kura za maoni zilizopigwa Agosti 4, 2025, ambapo alipata kura 5,690 na kuwashinda wagombea wengine tisa waliopitishwa na vikao vya juu vya uteuzi wa chama.


Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, amesema kati ya wagombea 24 waliochukua fomu, watatu ni wanawake na 21 ni wanaume.


“Wale wote tisa waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa pamoja na Hayati Ndugai wamechukua fomu. Pia, tunazo sura mpya 10 katika idadi hiyo,” amesema Mkaugala.

CCM Wilaya ya Kongwa ilitangaza kuanza upya mchakato wa kuchukua fomu Agosti 11, 2025, mara baada ya kumalizika kwa shughuli za maziko ya Hayati Ndugai.

Post a Comment

0 Comments