RC KENAN AKUNJUA MAKUCHA AMTUPA NJE MTENDAJI WA KATA ASIYESIKILIZA KERO ZA WANANCHI,ATATUA KERO KIBAO PAPO KWA HAPO ,ALIYEKWAMA LAKISITA YA MATIBABU ACHANGIWA CHAP, WANANCHI WAMSHANGILIA,

Na Joseph Ngilisho-ARUSHA

MKUU wa Mkoa wa Arusha , Kenani Kihongosi ameendesha mkutano wa hadhara uliowakutanisha mamia ya wakazi wa maeneo mbalimbali ili kusikiliza kero na changamoto zao, na mara moja, kuchukua hatua za kuzitatua ikiwa ni utekelezaji wa takwa la rais Samia Suluhu Hasan kuhakikisha wananchi wanaondokana na mzigo wa changamoto.


Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Soko kuu ,kata ya mjini Kati , ulihudhuriwa na wakuu wa idara, viongozi wa wilaya, na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za umma





Akizungumza leo agosti 12,2025 mbele ya wananchi, RC Kihongosi alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha serikali inasogea karibu na wananchi na kusikiliza changamoto zao moja kwa moja bila urasimu wowote.


Wakati wa usikilizaji wa kero hizo RC Kihongosi aliamuru Afisa mtendaji wa Kata  Simon ,Good luck Nnko ,kuondoshwa mara moja katika kituo  chake cha kazi  kwa kushindwa kusimamia vema majukumu yake ya kazi kwa wananchi.


>

“Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inalenga kusikiliza wananchi wake na kutatua matatizo kwa wakati. Ndio maana leo tumekuja na wataalamu wote ili kila kero ipate majibu hapa hapa ,” alisema RC.


Changamoto kubwa zilizotajwa na wananchi katika mkutano huo nyingi zilihusu watu binafsi hasa madai mbalimbali zikiwemo fedha ,ugumu wa maisha huku kero za kisekta zikiwa chache jambo linaloonesha wazi kuwa Serikali imepiga hatua.

Mara baada ya kusikiliza kero hizo, RC alitoa maelekezo kwa viongozi husika kutatua baadhi ya matatizo mara moja, huku mengine yakipangiwa muda maalum wa utekelezaji. Kwa mfano, kuhusu ubovu wa miundo  aliahidi kuondoka na kero hiyo.

Mwito wa Ushirikiano;

RC aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa za matatizo mapema na kushiriki katika shughuli za maendeleo huku alisisitiza suala zima la kulinda amani, kuepuka vurugu na maandamano yasiyo na tija.

>

“Maendeleo ya mkoa wetu hayataletwa na mtu mmoja, bali kwa ushirikiano wa kila mmoja wenu,” alisisitiza.


Awali RC Kihongosi kabla ya Mkutano huo wa hadhara alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo likiwemo jengo la utawala la jiji la Arusha.

Pia alitembelea jengo  la wagonjwa wa saratani linalojengwa kwa msaada wa mdau wa maendeleo kutoka kampuni ya Spanish Tiles pamoja na jengo la Benki ya damu salama linalotekelezwa na wadau wa sekta ya afya  katika hospitali ya Rufaa ya Mt Meru Mkoani Arusha.

 Jengo hilo linalenga kuboresha huduma za uchangiaji na upatikanaji wa damu salama kwa wakazi wa Jiji la Arusha na maeneo jirani.






Ends .

Post a Comment

0 Comments