By arushadigtal
Roman Starovoit (53), aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi wa Urusi, amekutwa amefariki dunia ndani ya gari lake nje kidogo ya jiji la Moscow. Mwili wake uligundulika ukiwa na jeraha la risasi, huku bastola yake binafsi ikipatikana karibu.
Tukio hili limetokea masaa machache tu baada ya Rais Vladimir Putin kutoa amri ya kumfuta kazi, ambapo hakueleza sababu rasmi ya hatua hiyo.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanahusisha tukio hilo na uchunguzi wa ufisadi unaohusiana na matumizi ya fedha kiasi cha rubles bilioni 19.4 (zaidi ya dola milioni 246) zilizotengwa mwaka 2022 kwa ajili ya kuimarisha mpaka wa Urusi na Ukraine katika eneo la Kursk – ambako Starovoit alikuwa kiongozi wa zamani.
Kwa miezi kadhaa, nafasi yake serikalini imekuwa ikihusishwa na tuhuma za ufujaji wa fedha hizo, jambo lililomweka kwenye presha kubwa kisiasa.
Kamati ya Upelelezi ya Urusi imethibitisha kuwa inaendelea kuchunguza mazingira ya kifo chake, ili kubaini kama kweli alijiua au kama kuna mkono wa mtu.
0 Comments