By arushadigtal
Rais wa Marekani, Donald Trump, amezua mjadala kwa kudai kuwa msanii maarufu Beyoncé alilipwa kimakosa kiasi cha dola milioni 11 ili kumuunga mkono mgombea urais wa Democratic, Kamala Harris, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Houston mwaka 2024.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na CNN na vyanzo vya uhakiki wa taarifa kama PolitiFact na FactCheck.org umebaini kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwepo kwa malipo hayo. Kumbukumbu rasmi za kampeni zinaonesha kuwa timu ya Harris ililipa kiasi cha dola 165,000 tu kwa kampuni ya utayarishaji inayohusiana na Beyoncé, kwa ajili ya maandalizi ya tukio hilo.
Mama wa Beyoncé, Tina Knowles, amekanusha vikali madai hayo, akieleza kuwa mwanaye hakupokea malipo yoyote kwa kushiriki tukio hilo.
Wataalamu wa sheria wamesisitiza kuwa hakuna sheria ya shirikisho inayokataza malipo kwa ajili ya ushiriki wa kisanii katika kampeni, lakini hakuna ushahidi kuwa Beyoncé alilipwa kama anavyodai Trump.
Licha ya kukosa ushahidi, Trump ameendelea kusisitiza kuwa Kamala Harris alivunja sheria na anapaswa kushitakiwa. Hadi sasa, hakuna uchunguzi rasmi uliothibitishwa dhidi ya Harris au Beyoncé.
0 Comments