By arushadigtal
Rais wa Kenya, William Ruto ameagiza polisi nchini Kenya kutumia nguvu zaidi dhidi ya watu wanaojihusisha na uporaji au uharibifu wa mali wakati wa maandamano, akisema kuwa wanaopatikana wakifanya vitendo hivyo wapigwe risasi kwenye miguu ili kudhibiti machafuko.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa nyumba za bei nafuu eneo la Kilimani, Nairobi, Ruto ameelezea masikitiko yake kuhusu kile alichokitaja kuwa ni hali ya kipekee ya vurugu na upinzani mkali dhidi ya serikali yake.
Alitilia shaka kwa nini viongozi wa upinzani wamekuwa wakionesha msimamo mkali dhidi yake tofauti na walivyofanya kwa marais waliomtangulia kama Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta.
Kwa mujibu wa Ruto, haieleweki ni kwa nini fujo na maandamano yanalengwa kwake binafsi, huku akisema kuwa si haki kuendeleza siasa za chuki, kiburi na ukabila.
0 Comments