MFANYABIASHARA SARAKIKYA ALITAKA JIMBO LA ARUMERU MASHABIKI,ADHAMIRIA KUUANGUSHA MBUYU ILI KUIKOMBOA JAMII YA WAMERU

Na Joseph Ngilisho- ARUMERU 

MfANYABIASHARA Maarufu wa Mazao , Johnson Exaud Sarakikya, leo Julai 01,2025 amerejesha fomu ya kuwania nafasi ya uteuzi wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), huku akimtanguliza mungu kujibu maombi yake, kwenda kuwatumikia watanzania waliopo katika jimbo la Arumeru Mashariki.


EXAUD akiwa na nia ya 'kuangusha Mbuyu' ni kijana aliyezaliwa katika jimbo hilo akidai ameguswa kwenda kuwatumikia watu wa Jamii ya Meru ambao wamekosa mwakilishi Sahihi.

Akiongea mara baada ya kurejesha fomu yake ,amedai amejipima na kujitathmini na kuamini anaweza kuwa chaguo la wana Meru ambao kwa muda mrefu amekosa mtu wa kumaliza changamoto  zao.

"Nimejipima na kujitathimini na kuona ninatosha na nina uwezo wa kujenga hoja kwa maneno ninao ,hivyo nikapata ujasiri wa kutaka kwenda kuwatumikia watanzania wenzangu katika jimbo la Arumeru Mashariki "

 "Ombi langu kwa wananchi muendelee kuniombea kwa mungu ili nivuke katika mchakato huu kwa kupata uteuzi ndani ya chama na jambo hili nalikabidhi mbele ya mungu kwa sababu ipo dhamira kubwa naiona mbele yangu kwa kijana mdogo kama mimi"Alisema 

Ends.. 

Post a Comment

0 Comments