TANAKI,SABAYA, NOAR, ELIAS NA MWAMBA SEVERE NANI MKALI WA JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI, 22 WACHUKUA NA KUREJESHA FOMU

 Na Joseph Ngilisho- ARUMERU 


LENGAI OLE SABAYA DC wa Zamani wa HAI Mkoani Kilimanjaro,amejeresha Fomu kwa kishindo na kuongeza joto la kinyang'anyiro cha kumpata mwakilishi sahihi wa jimbo la Arumeru Magharibi.

Ole sabaya ni Miongoni mwa Makada 22 waliochukua Fomu na wote 22 wamerejesha wakiwemo wanawake watatu wakianna shauku ya kupata uteuzi.

Sabaya ambaye aliambatana na mkewe akiwa kwenye gari zito la kifahari ,hakuwa tayari kuzungumza chochote wakati akirejesha Fomu hiyo na alilazimika kutimua mbio kuingia ndani ya ofisi kukwepa waandishi wa habari waliokuwa wameweka kambi katika ofisi za ccm wilaya ya Arumeru.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kisiasa katika jimbo hilo ,Sabaya anatajwa kama mwanasiasa mwenye uzoefu na uongozi ukizingatia aliwahi pia kuwa diwani katika jimbo hilo.

 "Sabaya ni kijana mchapakazi kwa kwwli mwenye nguvu na ushawishi wa wastani katika jimbo hilo ukizingatia kwamba jina lake ni kubwa na ni mtu mwenye misimamo Mikali "Alisema Mkazi qa eneo 


Baadhi ya watia nia wengine waliojitosa katika mbio hizo ni pamoja na Mbunge mtetezi wa jimbo hilo,NOAR LEMBRIS,ELIUS LUKUMAY,NOEL SEVERE NA JOHN TANAKI MSOMI WA CHUO KIKUU.











Post a Comment

0 Comments