MFANYABIASHARA KESSY ANYAKUA FOMU YA UBUNGE ARUSHA MJINI,AJIFANANISHA GOLIATHI NA MUSA

 Na Joseph Ngilisho-ARUSHA


MFANYABIASHARA VICTA KESSY amechukua fomu kwa lengo la kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini ,ili kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo .

"Nimechukua Fomu ya ubunge ili kuliongoza jimbo la Arusha mjini, nakuomba chama changu cha CCM Kuniamini ili waone nguvu ya uongozi"

"Najiamini katika maamuzi yangu ninachokiomba chama chagu kiniamini sina woga na yoyote aliyechukua Fomu namuamini aliyepo nyuma yangu"

Vickta Leonard  Kessy ni mfanyabiashara katika mikoa ya Arusha na dodoma na ni mara ya pili ya kuchukua Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa jimbo hilo la Arusha.

"Hao waliochukua fomu ni watu wa kawaida tu aliyepo nyuma yangu ni mkubwa kuliko wao kwa hiyo sina haja ya kuwaogopa, nayajua mahitaji ya watu wa Arusha"

"Mimi sio mara yangu ya kwanza kuchukua fomu mwaka 2020 nilifanya hivyo lakini sikufanikiwa,naamini katika falsafa ya uongozi maamuzi yanahitaji nguvu ya uongozi"

Aliongea hayo huku akijifananisha na historia ya Goriath na Daudi.

Enda..

Post a Comment

0 Comments