CCM YATANGAZA TAREHE YA KUANZA KULA VYA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE!

 By arushadigtal

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya uchujaji wa majina ya watia nia wake inayoanza kesho julai 4 hadi Julai 19, 2025.


Hatua hiyo ni baada ya kuhitimisha mchakato wa wanachama wake wa uchukuaji fomu  za kuomba ridhaa ya ubunge, uwakilishi na udiwani.


Katibu wa NEC, Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa,  Amos Makalla, akizungumza leo Julai 3, 2025, kuhusu mchakato uliohitimishwa wa uchukuaji fomu, amesema  

kuanzia kesho vikao vya uchujaji vinaanza ngazi ya kata.


“Vikao vya uchujaji vinaanza kwa maana tarehe 4, 2025, katika kata zetu wataanza kukaa kamati za siasa kutoa mapendekezo kwa ajili ya wagombea hawa kwa ajili ya uteuzi wa madiwani walioomba katika kata, viti maalum.



“kamati za siasa za mkoa kwa ratiba ya chama zinatarajia kukaa Julai 9, 2025, kufanya uteuzi kwa nafasi wanaoomba udiwani.


Makalla amesema kwa uwakilishi na ubunge uteuzi wa mwisho utafanywa na Kamati Kuu CCM. 


Amesema kwa mujibu wa ratiba yao, inaonesha ni Julai 19, 2025,  itafanya uteuzi wa mwisho kwa maana wagombea wale watatu watatu.


Post a Comment

0 Comments