MALI ZA BILIONEA WA MADINI IKIWEMO NYUMBA YA KULALA NA FAMILIA KUPIGWA MNADA , MAHAKAMA YASHIKILIA NYUMBA ZOTE DENI LAFIKIA MABILIONI YA FEDHA TAZAMA PICHA!

By arushadigtal 


MALI za Bilionea wa Madini jijini Arusha, Marehemu MATHIAS MANGA aliyefariki mwaka 2021,zinashikiliwa na mahakama na muda wowote zinaweza kupigwa mnada baada ya familia ya marehemu kushindwa kulipa deni linalotokana na Mkopo wa benki moja  nchini linalofikia kiasi cha dola za kimarekani milioni 6,sawa na zaidi ya bilioni  14 za kitanzania.







Taarifa zilizothibitishwa na dalali wa Mahakama ,Allan Mollel kupitia Kampuni yake ya First World Investment Court Broker ya jijini Arusha,anasema  kinachosubiriwa kwa sasa ni uthamini wa mali hizo (Valuation) ili mnada uweze kufanyika.


Hakuna aliyekuwa Tayari kuzungumzia kadhia hiyo akiwemo Mke wa Marehemu ambaye amekuwa hapokei simu yake ya mkononi na hajulikani alipo baada ya nyumba zake kuandikwa kwa kalamu NYEKUNDU kuwa zinashikiliwa na Mahakama ikiwemo nyumba ya kuishi iliyopo Ngarenaro NHC.


PIA JENGO la ghorofa 10 lililopo eneo la Sakina jijini hapa,ambalo bado halijakamilika nalo limeandikwa kwa maandishi hayo na dalali wa Mahakama jambo lililoshitua wakazi wengi wa jiji la Arusha kutokana  na umaarufu na heshima aliojijengea Mfanyabiashara huyo ambaye alifariki mwaka Agosti,2021.


Kesi hiyo ya madai ipo ngazi ya mahakama kuu kitendo cha Biashara jijini Dar es Salaam kwa hatua zaidi za utekelezaji.


Ends...








Post a Comment

0 Comments