ALLY BABU ATAKATA ARUSHA MJINI ,ATEULIWA KUGOMBEA UBUNGE ARUSHA MJINI AISHUKURU KAMATI KUU YA CCM KWA KUMWAMINI ,WEWE NANI USIMWAMINI!

Na Joseph Ngilisho- ARUSHA 

KADA Maarufu na Mzalendo jijini ARUSHA,ALLY BABU ameteuliwa kuwa mgombea Ubunge jimbo la ARUSHA mjini.BABU ni mkurugenzi wa kampuni ya BILSARM, mfanyabiashara na mkulima, ni miongoni mwa majina sita yaliyopitishwa na Kamati Kuu ya CCM kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini.


Babu, ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Arusha , amejipatia umaarufu kutokana na uzalendo wake wa kupenda kuchangia maendeleo kwa jamii na katika jiji la Arusha kupitia biashara zake.

Wakati akichukua na kurejesha aliahidi kuwapa zawadi ya maendeleo wakazi wa jimbo hilo na hawatajutia kumchagua.Ameishukuru halmashauri kuu kwa kurejesha jina lake kwa uaminifu.




Post a Comment

0 Comments