By arushadigtal
MAREKANI imeeleza kusikitishwa na taarifa za kuteswa nchini Tanzania kwa wanaharakati wawili wa Afrika Mashariki, Agather Atuhaire kutoka Uganda na Mkenya, Boniface Mwangi huku ikitoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa kina wa tuhuma hizi za ukiukaji wa haki za binadamu.
“Marekani imesikitishwa sana na taarifa za kuteswa nchini Tanzania kwa wanaharakati wawili wa Afrika Mashariki - Agather Atuhaire kutoka Uganda na Mkenya, Boniface Mwangi. Mwaka 2024 Atuhaire alitunukiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake Jasiri.
Tunatoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa kina wa tuhuma hizi za ukiukaji wa haki za binadamu. Tunatoa wito kwa nchi zote katika kanda hii kuwawajibisha wale wote wanaokiuka haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kufanya utesaji” imesema taarifa ya Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania.
0 Comments