LUKUMAY AVUTA UWEKEZAJI WA AFYA NA ELIMU KUTOKA LONDON
Na Joseph Ngilisho|Arushadigital
LONDON — Mbunge wa Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumay, ameanza jitihada mpya za kutafuta uwekezaji katika sekta za afya na elimu baada ya kufanya kikao muhimu na mdau wa NEPT-iNGO jijini London, Uingereza, leo Agosti 3, 2026.
Kikao hicho kiliazimia kuimarisha ushirikiano utakaowezesha uwekezaji wa miradi ya afya na elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha, huku Jimbo la Arumeru Magharibi likitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yatakayonufaika kwa kipaumbele.
Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuvutia wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi ili kuongeza ubora wa huduma za kijamii, hasa katika maeneo yanayohitaji miundombinu na huduma bora za afya pamoja na elimu.
Iwapo makubaliano hayo yatatekelezwa kama yalivyopangwa, yanatarajiwa kufungua fursa mpya za kuboresha maisha ya maelfu ya wakazi wa Arumeru Magharibi na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Ends


Post a Comment