KILIO WANAWAKE WAZIMIA WAKILILIA NYAMA OLASITI , BODI YA NYAMA IKIZUIA UCHINJAJI WA KONDOO WA MSAADA WALIOTOLEWA NA MWARABU

TAHARUKI OLASITI BAADA YA BODI YA NYAMA KUSITISHA UCHINJAJI WA KONDOO

Na Joseph Ngilisho- Arusha Digital | ARUSHA

Hali ya taharuki na sintofahamu imeibuka miongoni mwa wananchi wa Kata ya Olasiti, jijini Arusha, kufuatia uamuzi wa Bodi ya Nyama kusitisha shughuli za uchinjaji wa kondoo ambazo zimekuwa zikifanyika katika eneo hilo kwa kipindi kirefu.

Wananchi wanaotegemea huduma hiyo wamesema hatua hiyo imewaathiri kwa kiasi kikubwa, wakieleza kuwa nyama ya kondoo ilikuwa chanzo muhimu cha chakula kwa familia nyingi pamoja na kuwawezesha baadhi ya wananchi kujipatia kipato kupitia shughuli zinazohusiana na biashara ya nyama.

"Mmoja ya wanawake waliofika katika tukio hilo,Aisha Bakari alisema kuwa amefika kuchukua nyama ambazo hutolewa sadaka na msamalia na yeye hana msaidizi hivyo kuzuia kuchinjwa kwa Kondoo kumnyima haki ya masingi ya kupata kitoweo"

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wameeleza kuwa huduma hiyo imekuwepo kwa zaidi ya miaka mitano bila kuwepo kwa changamoto kubwa zilizoripotiwa, jambo ambalo limewafanya kushangazwa na uamuzi wa kusitishwa kwake ghafla.

Wamesema kusimamishwa kwa shughuli hizo kumeibua maswali mengi kuhusu sababu zilizochangia hatua hiyo, huku wakihofia athari za kiuchumi na kijamii zinazoweza kujitokeza iwapo suluhisho la haraka halitapatikana.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wameziomba mamlaka husika kufanya tathmini ya kina kuhusu suala hilo na kutoa ufafanuzi rasmi ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza.

Aidha, wameitaka Serikali na wadau wa sekta ya mifugo kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto zilizopo bila kuathiri mahitaji ya wananchi wanaotegemea huduma hiyo katika maisha yao ya kila siku.

Ends. 

Post a Comment

أحدث أقدم