By Arusha Digital — MOSHI
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo maarufu kama Ibraline, amenusurika kifo kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Kirinjiko, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Ajali hiyo ilitokea Februari 18, 2026 wakati Mbunge huyo akiwa kwenye msafara uliokuwa ukihusiana na ziara ya Mwigulu Lameck Nchemba.
Manusura wa Ajali
Mbali na Mbunge Shayo, manusura wengine waliokuwemo kwenye gari hilo ni dereva wake pamoja na katibu wake. Taarifa za awali zinaeleza kuwa wote walinusurika bila kupoteza maisha, huku hali zao zikiendelea kufuatiliwa.
Polisi Waanza Kufuatilia Tukio
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema bado hajapokea taarifa rasmi ya ajali hiyo kutoka kwa maafisa wa usalama barabarani.
“Nami nimesikia taarifa hiyo, nipeni muda nifuatilie kwa RTO, nitawarudia,” amesema Kamanda Maigwa.
Uchunguzi Unaendelea
Jeshi la Polisi linatarajiwa kutoa taarifa kamili mara baada ya kukamilisha uchunguzi wa awali kuhusu chanzo cha ajali hiyo, huku wananchi na wadau wa siasa wakionyesha wasiwasi na kutuma salamu za pole kwa Mbunge huyo na manusura wengine.
Ends..










0 Comments