WAANDISHI WA HABARI TANZANIA WASHIRIKI MAFUNZO YA USALAMA BAADA YA UCHAGUZI
Na Joseph Ngilisho – Arusha
Kamati ya Mipaka, kwa kushirikiana na Taasisi ya Waandishi wa Habari (MAIPAC) inayojihusisha na teknolojia na uandishi wa habari, imeandaa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Arusha yakijumuisha masuala ya usalama, uandishi wa habari katika migogoro, na kuimarisha amani katika jamii.
Mafunzo haya, yaliyoshirikisha waandishi 35 kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Geita, Mara, Mwanza, Manyara, na wenyeji wa Arusha, yalilenga kuandaa waandishi kushughulikia changamoto zilizoweza kutokea baada ya uchaguzi, kutoa mazoezi ya vitendo, na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma.
Waandishi walipatiwa nafasi ya kushirikiana changamoto wanazokabiliana nazo, hasa wakati wa ripoti hatarishi za kisiasa.
Mafunzo pia yalijumuisha masuala ya kisheria yanayohusiana na tasnia ya habari, ikiwemo haki za waandishi, matamko yanayolinda wahariri, na fursa za kupata usalama wa kisheria na kinga dhidi ya vitisho.
Mafunzo yalisisitiza umuhimu wa kuunganisha nguvu, kushirikiana na wadau, na kujenga mitandao ya usaidizi ili kupunguza hatari zinazoweza kutokea katika shughuli za uandishi.
Shirika la Press Limited lenye makao makuu nchini Uholanzi, pamoja na wadau wengine wa ndani na wa kimataifa, limeonyesha umuhimu wa kuendeleza mafunzo kama haya. Lengo ni kuimarisha ujuzi wa waandishi, kuhakikisha wanaripoti kwa usahihi, na kujikinga na vizuizi vya kisheria, afya ya akili, na maadili.
Alisema baada ya uchaguzi, baadhi ya waandishi walikumbana na changamoto za kurudi kazini kutokana na hofu na hatari zinazohusiana na ripoti za kisiasa. Mafunzo haya yamewawezesha kutambua fursa za kisheria, jinsi ya kutumia sheria zinazolinda haki zao, na namna ya kushirikiana kupata msaada wa kisheria iwapo wanakabiliwa na mateso au ukandamizaji.
"Baada ya uchaguzi wa Oktoba 29,2025 tulishuhudia mambo mengi yalitokea na wandishi wengi walipata Madhira na vitisho tukaona ni muhimu kuwakutanisha ili kubadilishana changamoto na kupata uzoefu wa kila mmoja hasa masuala ya kisheria,ukizingatia kwamba wandishi wengi walishuhudia mauaji,majeruhi na vipigo na kupata matatizo ya Trauma"Alisema
Katika Mafunzo hayo imethibitisha kwamba kuna sheria nyingi zinazolinda haki za waandishi, na matamko ya kitaifa na kimataifa yanaweza kusaidia kuimarisha usalama wao. Pia yameonesha umuhimu wa kushirikiana, kubadilishana uzoefu, na kujenga utaratibu wa usaidizi katika kukabiliana na migogoro inayoweza kutokea baada ya uchaguzi au katika matukio ya kijamii.
Musa Juma, Mkurugenzi wa Taasisi ya Waandishi wa Habari, amesema:
"Tunaona ni muhimu kwa waandishi wa habari kushirikiana na kusaidia jamii za pembezoni. Kupitia mafunzo na ushirikiano wa kijamii, tunalenga kuwawezesha waandishi kuripoti kwa usahihi, kujilinda kisheria, na kutoa taarifa zinazosaidia kuimarisha amani na usalama katika jamii."
Mafunzo haya yanathibitisha jitihada za kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari nchini Tanzania na kutoa mwongozo wa jinsi waandishi wanavyoweza kujilinda kisheria na kimaakili wakati wa ripoti hatarishi."Alisema
Mwisho














0 Comments